
MagerezaTanzania
925 subscribers
About MagerezaTanzania
📍CHANNEL RASMI YA JESHI LA MAGEREZA TANZANIA BARA. 📍Est. Agosti 25, 1931 📍P. O. Box 1176, Msalato, Dodoma-Tanzania. 🌐www.magereza.go.tz 📩[email protected]
Similar Channels
Swipe to see more
Posts

Fuatilia hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia YouTube yetu.

MAAFISA SHERIA NA UREKEBU JESHI LA MAGEREZA 'WAPIGWA MSASA' MKOANI MOROGORO. Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza (CP) Nicodemus Tenga, leo Juni 09, 2025 ameongoza kipindi maalum cha majadiliano kuhusu mambo mbalimbali ya Kisheria ikiwemo mapokezi ya wafungwa na hesabu za kifungo, ikiwa ni siku moja kuelekea ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Maafisa Sheria na Maafisa Urekebu wa Jeshi la Magereza, kuhusu Huduma za Msaada wa Kisheria, Mapokezi ya Wafungwa Magerezani na adhabu mbadala, katika Ukumbi wa Mikutano wa Cate Hoteli mkoani Morogoro. Mafunzo hayo ya siku tano yameandaliwa na Wizara ya Katiba na Sheria ambapo yatafunguliwa rasmi Juni 10, 2025 na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Eliakim Chacha Maswi.

#magerezaupdates🇹🇿 Ziara ya Mhe. Innocent Lugha Bashungwa, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Msalato jijini Dodoma, Februari 14, 2025.