SUCCESS FOR FUTURE🤗 WhatsApp Channel

SUCCESS FOR FUTURE🤗

1 subscribers

About SUCCESS FOR FUTURE🤗

Successful journey in life should be shared together. The Philosophy of Life in beings and beyond the beings.

Similar Channels

Swipe to see more

Posts

SUCCESS FOR FUTURE🤗
SUCCESS FOR FUTURE🤗
2/8/2025, 6:44:48 AM

*ANAYEJIFUNZA HASHINDWI KAMWE.* _Kuacha kujifunza ni kuandaa kushindwa._ Rafiki yangu mpendwa, mambo mengi ambayo tumekuwa tukihangaika nayo kila mara, ndiyo yanayotupa picha halisi ya sisi. Tangu ulipokuwa mdogo hadi ulipo sasa, ni dhahiri kuwa kuna vitu vingi ambavyo ulikuwa unahangaika navyo na hadi sasa bado unahitajika kufanya. Kilichokuwa cha muhimu zaidi ya vyote kilikuwa kujifunza. Kila tunachokijua katika kila sehemu ya maisha kimetokana na kujifunza, aidha tabia au mitazamo ambayo inaweza ikawa tumejifunza kwa kuiga au kwa uzoefu. Kujifunza katika kitu chochote ambacho huwa kinakupa changamoto, iwe katika kazi, maendeleo binafsi na maisha ya kawaida kwa ujumla. Kila anayetumia kila muda wake kujifunza, uwezekano wa kushindwa katika mambo mengi ni mdogo sana. Kwasababu, ataweza kutatua changamoto ambazo zinawakabili wengine, kuona fursa ambazo wengine hawazioni, pia kuwa na uwezo wa kuishi katika mazingira ambayo wengine wanashindwa kuishi kwa kutumia rasilimali zilizopo. Ni ukweli ulio wazi kuwa, kila ambaye hajifunzi anajiandaa kushindwa katika maisha yake yote. Ukiachana na siku masaa hata miaka, kila sekunde huwa ni tofauti. Mfano mzuri ni katika hali ya afya ambayo inaweza kuwa tofauti kwa dakika hadi dakika, pia katika hali ya hewa ambayo kwa asili inaweza kubadilika wakati wowote. Hii inaweka wazi kuwa bila kujifunza unajiandalia kuanguka vibaya, na kujiweka katika dhiki kubwa ya kupitwa na wakati. Bila kujifunza unapitwa na wakati, na hii ni kila siku na kila sekunde. Pata picha mtu ambaye amekaa miaka 10 bila kujifunza leo angekuwa anaongea nini? Ni wazi kuwa atakacho kiongea sasa kitakuwa kimepitwa na wakati. Pata picha ungeacha kujifunza vyote ulivyojifunza toka mwaka 2015 ambapo imepita miaka 10 tu. Nafikiri usingekuwa hapo ulipo sasa. Fikiria faida iliyopo katika kujifunza vitu vipya kila siku. Swali kubwa lipo katika vitu vya kujifunza. Ni vitu gani vya kujifunza? Vipo vingi sana ambavyo ni vipya vinavyotokea kila mara lakini, siyo kila kitu unapaswa kuwa nacho. Vipo ambavyo vinaweza kukufanya kuwa bora kuliko ulivyokuwa na kuwa vibaya zaidi ya ulivyokuwa. Unapaswa kutambua unachokitaka na ambacho kipo ndani ya maadili yako, tofauti na kujifunza kila kitu. Sikiliza sauti yako ya ndani ambayo daima inasema ukweli kuhusu wewe, na yenyewe itakufunulia yote. Ukilinganisha na vurugu nyingi katika zama hizi, ambapo kwa sasa kila mtu anatetea kile anachokifanya, kila mtu anahitaji wafuasi. Mtu pekee wa kumsikiliza ni wewe mwenyewe kwa sababu ni vigumu na kamwe huwezi kujidanganya mwenyewe. Kama ilivyo katika kula chakula, ukiacha kula kila siku unajiandaa kufa kwa siku zijazo. Vivyo hivyo, kuacha kujifunza kila siku ni kujiandaa kushindwa. Binafsi kama ingekuwa kuandika kuhusu kujifunza, ningeandika maelezo ambayo hayawezi kuwa na hitimisho. Ujumbe wa kuondoka nao hapa ni *"Kujiandaa kushinda katika kila kitu kwa kujifunza"* Zipo namna nyingi ambazo watu huwa tunajifunza, wengine wanatumia makosa yao wenyewe, wengine kwa kusoma vitabu kupata uzoefu kutoka maisha ya watu wengine walioishi kabla yetu, wengine mazingira waliyo kulia au kuishi n.k. Angalia namna unavyojifunza sasa na ulivyojifunza vitu unavyojua, kuanzia lugha yako ya kwanza uliyojifunza. ©Inocent Herman, Mwalimu mwenye mapenzi makubwa katika taaluma yake. https://t.me/SuccessForTheFuture

Link copied to clipboard!