Find WhatsApp Channels

Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.

Channels & Posts for #airlinerevenue

Posts

Aviation Tanzania on Instagram: "Kenya Airways yapata Bilioni 4.6 kutokana na tiketi zilizoisha muda bila kutumiwa na abiria. Shirika la ndege la Kenya Airways limeingiza mapato ya kiasi cha shilingi bilioni 4.6 kutokana na tiketi ambazo hazikutumika ndani ya kipindi cha miezi 13 tangu ziliponunuliwa na abiria. Taarifa ya shirika hilo imeonesha kuwa mapato yakiyotokana na tiketi zilizopitwa na muda yameongezeka kwa asilimia 9.4 kutoka bilioni 4.2 mwaka uliopita, ikiwa ni kiwango cha juu zaidi kuwahi kufikiwa katika kipindi cha miaka mitano. Kwa kawaida, Kenya Airways huuza tiketi mapema na huzihesabu kama madeni ya muda mfupi kwenye vitabu vyao vya fedha. Tiketi hizo hubadilika na kuwa mapato halali iwapo abiria atasafiri au atashindwa kusafiri ndani ya muda wa mwaka mmoja. Mkuu wa Idara ya Bei na Usimamizi wa Mapato katika shirika hilo, Jackson Kamande, amesema kuwa sera ya matumizi ya tiketi ya shirika hilo inalingana na viwango vya kimataifa, ambapo tiketi huwa halali kwa kipindi cha miezi 12 hadi 13 tangu zinunuliwe. Ongezeko hili la mapato limetokana na ongezeko la safari na uwekaji nafasi za tiketi kutoka kwa wateja wa shirika hilo. Chanzo-NTV Kenya #airlinerevenue #kenyaairways #kq #airlinepassengers #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/p/DKMYnRpMAcq/?igsh=OGhhb2l6emEwaWsx *Kenya Airways yapata Bilioni 4.6 ku...