Find WhatsApp Channels

Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.

Channels & Posts for #catctanzania

Posts

Aviation Tanzania on Instagram: "Chuo cha Mafunzo ya Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) kinatarajia kuanza awamu mpya ya mafunzo ya urushaji wa ndege nyuki (drones) kuanzia April, 8, 2025. Mafunzo haya yanalenga kuwapa washiriki ujuzi wa kitaalamu katika uendeshaji wa ndege zisizo na rubani, ambazo zinazidi kutumika katika sekta mbalimbali kama sekta ya usalama, kilimo, utafiti na usafirishaji wa mizigo midogo. Kwa mujibu wa CATC, mafunzo haya yatadumu kwa muda wa wiki nne na gharama ya ada ni Shilingi milioni 1.4 za Kitanzania. Mbali na gharama za ada, mshiriki atatakiwa kulipia gharama za vipimo vya kiafya ambavyo atatakiwa kuvifanya kabla ya kuanza mafunzo. Mafunzo haya yanatarajiwa kusaidia kuongeza idadi ya marubani wa ndege nyuki waliobobea, kuendana na maendeleo ya teknolojia ya anga nchini Tanzania. #aviationtraining #dronepilot #catctanzania #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviationcareer #aviationtanzania✈ #aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviatatv"

https://www.instagram.com/p/DGXRyhftJbJ/?igsh=c2p4b280a3gyYngw *Chuo cha Mafunzo ya Usafiri wa Ang...