Find WhatsApp Channels

Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.

Channels & Posts for #deathonboard

Posts

Aviation Tanzania on Instagram: "Wanandoa wadai kulazimishwa kukaa pembeni ya mwili wa marehemu kwa masaa manne ndani ya ndege. Wanandoa wawili, Mitchell Ring na Jennifer Colin wamedai kuwa walilazimishwa kukaa kwa masaa manne pembeni ya mwili wa mwanamke aliyefariki kwenye ndege ya Qatar Airways iliyokuwa ikisafiri kutoka Australia hadi Qatar. Wanandoa hao walikuwa wakitokea Melbourne kuelekea Doha, mji mkuu wa Qatar, wiki iliyopita, masaa kumi baada ya ndege hiyo kuanza safari, mwanamke mmoja alitoka ndani ya choo na kuanguka kisha kupoteza maisha mbele yao. Wawili hao walieleza kwenye kipindi cha habari cha Australia “A Current Affair” siku ya Jumapili kuwa walifanya kila jitihada kuokoa maisha ya mwanamke yule, lakini ilishindikana, jambo ambalo lilikuwa gumu kutazama, alisema Ring. Ring alisema wafanyakazi wa ndege waliuweka mwili wa mwanamke huyo kwenye kiti kilichokuwa wazi karibu nao kwa masaa manne yaliyosalia ya safari yao. Walieleza kuwa,Bi.Jeniffer alikuwa pembeni ya mumewe Ring, wakiwa kwenye mstari wa viti vinne wahudumu walimwambia Jennifer ahamie upande wa pili wa mumewe naye alikubali bila shida, kisha wakauweka mwili wa mwanamke huyo kwenye kiti alichokuwa amekaa Jennifer mwanzoni. Wanandoa hao walisema wafanyakazi wa ndege hawakuwaruhusu kubadilisha viti kwa kipindi chote cha safari na waliwaomba wabaki kwenye viti walivyokuwa hadi wahudumu wa matibabu walipowasili. Qatar Airways, ambayo inamilikiwa na serikali ya Qatar, ilitoa taarifa siku ya Jumatatu ikitoa pole kwa familia ya abiria ambaye alifariki ndani ya ndege yao kwa bahati mbaya. Waliomba msamaha kwa usumbufu wowote uliojitokeza katika tukio hilo, na walikuwa kwenye mchakato wa kuwasiliana na abiria kulingana na sera na taratibu zao. . Chanzo-NBC News #qatarairways #deathonboard #aviationtanzania✈️ #AviationTanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviationtanzania✈ #aviatamedia"

https://www.instagram.com/p/DGiE2VutzUF/?igsh=NmRhc29sdmxlZDB6 *Wanandoa wadai kulazimishwa kukaa p...