Find WhatsApp Channels
Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.
Channels & Posts for #fatherswings
Posts
Aviation Tanzania on Instagram: "Ndoto ya urubani ya Fiona Austin ilivyohamasishwa na baba yake ambaye ni rubani Mstaafu. Fiona Austin-McDonald ambaye kwa sasa ni rubani msaidizi (First Officer) amefuata nyayo za baba yake, Wade Austin-McDonald, rubani aliyestaafu mwaka 2020 baada ya kuhudumu kwenye sekta ya anga kwa zaidi ya miaka 44. Tangu alipokuwa mtoto, Fiona alihamasishwa na mapenzi aliyokuwa nayo baba yake katika fani ya urubani, lakini safari ya Fiona katika fani ya urubani haikuwa rahisi. Katika mahojiano na chombo cha habari cha "Because of Them We Can", Fiona alieleza kuwa ingawa baba yake alimpa msukumo mkubwa,lakini hatua halisi ya kuamua kuwa rubani ilikuja baada ya yeye mwenyewe kushuhudia mwanamke akiendesha ndege kwa mara ya kwanza alipokuwa mfanyakazi wa ndani ya ndege (Flight Attendant). Alisema kuwa hiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kuona mwanamke katika chumba cha marubani, na hapo ndipo alipotambua kuwa hata yeye angeweza kuwa sehemu ya tasnia hiyo. Fiona na baba yake wamewahi kurusha ndege pamoja mara kadhaa, ikiwa ni pamoja na safari iliyofanyika kutoka Antigua hadi St. Kitts na St. Maarten. Lakini kilichogusa moyo wake zaidi ni fursa aliyopata ya kufundishwa na baba yake wakati wa mafunzo yake ya kwanza ya urubani wa kibiashara (Commercial Pilot). Alisema kuwa lilikuwa jambo la kipekee kwake na kwamba alijitahidi kuonekana mtulivu ili aweze kutekeleza majukumu yake vizuri, ingawa ndani yake alihisi fahari kubwa. Kwa upande wake, Wade Austin-McDonald, ambaye amehudumu kama rubani wa ndege za kibiashara "Commercial Pilot" kwa zaidi ya miaka 40, alifurahia sana kurusha ndege pamoja na binti yake. Alieleza kuwa hilo lilikuwa tukio lenye hisia kali kwake, na ingawa alijizuia kuonyesha msisimko, alijawa na furaha na fahari kubwa kama baba. Fiona amewahi kumuelezea baba yake kama mtu mwenye mchango mkubwa katika fani ya urubani katika mji wa Caribbean, akiwafundisha marubani wengi ambao baadaye walifanikiwa katika taaluma hiyo huku akiongeza kuwa yeye mwenyewe ni sehemu ya urithi huo wa baba yake. Baada ya kustaafu, Wade aliendelea kuwa katika sekta ya anga kama mkaguzi wa shughuli za ndege. . #familypilots #pilot #firstofficer #fatherswings #aviationcareer #"
https://www.instagram.com/p/DF7Xws9NOTY/?igsh=ZmJkNmxwNWVqdnFt *Ndoto ya urubani ya Fiona Austin i...