Find WhatsApp Channels

Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.

Channels & Posts for #flightincident

Posts

Aviation Tanzania on Instagram: "Njiwa wachelewesha safari ya ndege ya Delta Airlines. Safari ya ndege ya abiria ya Delta Airlines aina ya Airbus A220-300 ilichelewa kuanza kwa wakati baada ya njiwa wawili kuonekana wakiruka ndani ya ndege hiyo katika Uwanja wa Ndege wa Minneapolis nchini Marekani. Njiwa wa kwanza alibainika wakati ambao abiria walikuwa wakiingia ndani ya ndege, ndipo mfanyakazi wa shirika hilo alifanikiwa kumtoa ndege huyo nje kabla ya safari kuanza. Hata hivyo,kabla ya ndege kuanza kuruka, njiwa wa pili alionekana akiruka ndani ya ndege, kwa kuzingatia usalama wa abiria na wafanyakazi, rubani aliamua kuirudisha ndege hiyo kwenye lango la maegesho. Mafundi wa shirika hilo waliingia ndani ya ndege na kumtoa njiwa wa pili na hakuna mtu aliyejeruhiwa na ndege haikupata uharibifu wowote. #flightincident #deltaairlines #a220 #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/reel/DKL89b2MeUE/?igsh=YmtpbzE1aHV1eHgx *Njiwa wachelewesha safari ya nde...