Find WhatsApp Channels
Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.
Channels & Posts for #miamiinternationalairport
Posts
Aviation Tanzania on Instagram: "Polisi wamdhibiti mwanaume aliyekuwa akiwashambulia maafisa wa usalama katika uwanja wa ndege wa Miami. Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 28 kutoka Toronto, Kanada,amekamatwa na polisi baada ya kuanzisha vurugu na kuwashambulia maafisa wa usalama wa usafiri wa anga (TSA) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Miami. Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, tukio hilo lilitokea saa moja asubuhi katika eneo la ukaguzi wa usalama ambapo mwanaume huyo, aitwaye Cameron Dylan McDougall, alianza kwa kumshambulia abiria mwenzake, kabla ya kuhamia kwa maafisa wa TSA waliokuwa kazini. Video ya usalama inaonesha McDougall akijaribu kumpiga afisa mmoja wa TSA kwa ngumi, kisha kumshika mikono na kuendelea kujaribu kumpiga. Alipojikwaa na kuanguka, afisa mwingine wa TSA alimshika miguuni ili kumzuia. Wakati wakijaribu kumdhibiti, McDougall alimpiga afisa mmoja ngumi tatu usoni. Mashuhuda wa tukio hilo walimshikilia McDougall hadi maafisa wa usalama walipowasili na kumtia mbaroni. McDougall sasa anakabiliwa na mashtaka kadhaa, yakiwemo kumpiga afisa wa usalama na mtumishi wa serikali, kumpiga mtu mwenye umri wa miaka 65, na kosa la kushambulia mtu mwingine. #airport #tsa #miamiinternationalairport #unrulypassenger #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"
https://www.instagram.com/reel/DKPOrLwMUyj/?igsh=MTBvdmp2Z3F3aDE0cA== *Polisi wamdhibiti mwanaume a...