Find WhatsApp Channels

Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.

Channels & Posts for #parentalcare

Posts

Aviation Tanzania on Instagram: "Kwa wazazi wengi, yawezekana ni changamoto kubwa kupata muda wa kutosha kuwa na familia kutokana na majukumu mengi ya kikazi kila siku. Lakini kwa Racheal Kaur, mama mwenye asili ya India anayeishi nchini Malaysia, changamoto hii ameipatia suluhisho la kipekee ambapo husafiri kwa ndege kila siku kwenda kazini na kurudi nyumbani. Kaur, ambaye ni meneja msaidizi wa fedha katika kampuni ya ndege ya AirAsia, huamka saa 10 alfajiri na kuelekea uwanja wa ndege kwa safari ya saa moja kutoka Penang hadi Kuala Lumpur. Kufikia saa 1:45 asubuhi, anakuwa ofisini tayari kwa kazi. Jioni, hupanda ndege kurudi nyumbani, na hufika saa 2 usiku, muda mzuri wa kutumia na watoto wake wawili wenye umri wa miaka 12 na 11. Awali, Kaur aliishi Kuala Lumpur ili kuwa karibu na eneo la kazi, lakini kuwa mbali na familia kulimfanya afikirie upya mpangilio wake wa maisha ndipo mwaka 2024, alipoamua kuanza kufanya safari za ndege kila siku badala ya kukaa mbali na familia yake. Cha kushangaza ni kuwa, safari yake ya kilomita 350 kila siku sio tu kwamba imerahisisha uwiano wa kazi na familia, bali pia imemsaidia kupunguza gharama za maisha. Badala ya kulipa kodi ya nyumba na gharama za chakula katika mji wa Kuala Lumpur kiasi cha $474, sasa anatumia takriban $316 kwa mwezi. Pamoja na ratiba yake ngumu, Kaur anasema safari zake za ndege zinampa muda wa kipekee, akitumia fursa hiyo kusikiliza muziki na kutazama mandhari nzuri kutoka angani. Ingawa kazi ya mbali ingeonekana kuwa na suluhisho rahisi ambalo ni kufanyia kazinyumbani, lakini yeye alieleza kuwa anapendelea mazingira ya ofisini yanayomuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa. Licha ya uchovu wa safari za kila siku, Kaur anasema kuwa kila kitu kinakuwa na maana anapofika nyumbani na kuwaona watoto wake. . #parentalcare #aviationtanzaniaupdates #airasia #aviataupdates #aviatamedia #aviationcareer #aviationtanzania✈ #aviata"

https://www.instagram.com/p/DGfECpvto1G/?igsh=OTlwbnZ5bjE1bG1z *Mwanamke anayesafiri Km 350 kwa nde...