Find WhatsApp Channels
Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.
Channels & Posts for #passengerexperience
Posts
Aviation Tanzania on Instagram: "Utalipia $14,000 kwa Saa moja kuwa ndani ya ndege ya kifahari iliyopambwa kama hoteli ya nyota Tano. Jiji la Dubai linaendelea kuwa kitovu cha starehe na maisha ya kifahari na hivi sasa ndani ya jiji hilo,kuna huduma ya kipekee ya ndege binafsi inayokodishwa kwaajili ya sherehe zinazofanyika angani. Ni ndege binafsi inayomilikiwa na Kabir Mulchandani,mmiliki wa hoteli za FIVE Hotels and Resorts, iliyopambwa katika mandhari ya kifahari kama hoteli, na hukodishwa kwa sherehe au safari binafsi za anga. Ndege hii ina uwezo wa kubeba watu 16 na imepambwa na vifaa vya kisasa kama taa za LED, mfumo wa sauti wa kiwango cha kumbi za starehe, runinga kubwa, kitanda cha kifalme na bafu la ndani, mandhari Sawa na ilivyo katika hoteli za kifahari. Kwa gharama ya dola 14,000 kwa saa moja, mtu yeyote anaweza kukodisha ndege hii kwa ajili ya sherehe au safari za kifahari, hata kama hatumii huduma ya hoteli. Ndege hii, inayoitwa 9H-FIVE, ni mfano wa Airbus ACJ 220 na inafanya safari zake kwenda maeneo kama Santorini, Ibiza, au Zurich. Mwanzilishi wa FIVE Hotels, anasema huduma hii ni njia ya kuwapatia wateja huduma ya kipekee na yenye kukumbukwa. #5starhotels #fivehoteldubai #passengerexperience #airbusacj220 #9hfive #aviationlovers #aviationtanzaniaupdates #aviationtanzaniaupdates #aviata"
https://www.instagram.com/p/DKW8t3sMeZe/?igsh=MTFydThrbGc1ZXZpbw== *Utalipia $14,000 kwa Saa moja k...