Find WhatsApp Channels

Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.

Channels & Posts for #passengerseat

Posts

Aviation Tanzania on Instagram: "Wakati abiria wengi wanaotumia usafiri wa anga hutumia siti moja pekee kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine, hii ni tofauti kwa Rumeysa Gelgi, raia wa Uturuki ambaye anavunja rekodi ya dunia (Guinness World Records) kwa kuwa mwanamke mrefu zaidi duniani. Rumeysa Gelgi, ambaye ana urefu wa futi 7 na inchi 0.7 (sawa na mita 2.15), amefichua kuwa kila anaposafiri kwa ndege hulazimika kulipia siti sita kutokana na hali yake ya kiafya inayomlazimu kulala kwenye machela wakati wote wa safari. Gelgi, ambaye anaishi katika jimbo la Karabük, kaskazini mwa Uturuki, anasumbuliwa na ugonjwa nadra unaojulikana kama Weaver syndrome, hali inayosababisha ukuaji wa haraka wa mwili pamoja na changamoto nyingine za kiafya. Kwa sababu ya urefu wake wa kipekee, amekuwa akitegemea kiti cha magurudumu. Kwa miaka mingi, alikuwa hawezi kabisa kusafiri kwa ndege kutokana na kutokuwepo kwa nafasi ya kutosha. Lakini kupitia Shirika la Ndege la Turkish Airlines, sasa anaweza kusafiri kimataifa baada ya shirika hilo kuondoa siti sita katika ndege moja na kuweka machela maalum kwa ajili yake. Safari yake ya kwanza ya anga ilifanyika mwezi Septemba mwaka 2022 kutoka San Francisco hadi Istanbul. Aliielezea safari hiyo kama “safari kamili na isiyo na dosari.” Tangu wakati huo, Rumeysa amekuwa akisafiri angalau mara moja kila mwaka, lakini ni kwa kutumia shirika lake la taifa pekee, ambalo lina uwezo wa kutoa huduma hiyo maalum. Licha ya kuwa tayari ametembelea mataifa kama Marekani, Uingereza, Hispania na Italia, kila safari huambatana na maandalizi makubwa na gharama kubwa. Mbali na kulipia nafasi ya machela ambayo ni sawa na siti sita za abiria wengine, anahitajika kufika uwanja wa ndege saa nne kabla ya muda wa safari kwa ajili ya kukutana na wataalamu wa afya na maandalizi mengine ya usalama. Hadi sasa, hajawahi kusafiri kwa basi au treni, lakini ana matumaini ya kufanya hivyo katika miezi ijayo. Katika mahojiano na Luxury Travel Daily, Rumeysa alieleza jinsi anavyoumizwa na hali ya kushindwa kutembelea maeneo yenye historia ya kuvutia kutokana na ukosefu wa njia salama. Kutokana na uwepo wa vyuma vya msaada mgongoni mwake, hata kuanguka kidogo inaweza kuwa hatari kubwa kwake."

https://www.instagram.com/reel/DKwGwSJNs21/?igsh=MzhvcnNoMzhmOHpp *Mwanamke mrefu zaidi duniani hul...