Find WhatsApp Channels

Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.

Channels & Posts for #shada

Posts

Aviation Tanzania on Instagram: "Mwaka 2023, mama mmoja kutoka Ethiopia aitwaye Minalu Mergiya ilivutia watu wengi duniani kutokana na hadithi yake ya kusisimua. Kwa zaidi ya miaka 30, aliishi na kufanya kazi ya ndani nchini Lebanon ili kumsaidia mwanawe afikie ndoto yake ya kuwa rubani. Minalu Mergiya, alihamia Lebanon miaka ya 1990 akiwa na ndoto moja kubwa: kumpa mwanawe maisha bora. Kwa miaka 30, Minalu alifanya kazi kama mfanyakazi wa ndani katika familia mbalimbali, akihangaika siku zote kumlipia mwanawe ada ya shule na kumtunza akiwa mbali. Mwanawe, Kirubel Salomon, alipokuwa mdogo, alitamani kuwa rubani, ndoto ambayo mama yake aliichukulia kwa uzito mkubwa.Wakati Minalu alipokuwa mbali na mwanae waliwasiliana kwa barua Mara kadhaa, akimtia moyo katika kila hatua ya maisha. Na juhudi hizo hazikuenda bure: Kirubel alifanikiwa kujiunga na masomo ya urubani na hatimaye kuwa rubani wa shirika la ndege la Ethiopian Airlines, shirika kubwa na maarufu zaidi la ndege barani Afrika. Miaka mingi ilipita tangu Minalu atembelee nchini Ethiopia. Lakini siku moja, alifunga safari ya kurejea nyumbani, safari ambayo haikuwa ya kawaida. Bila kujua, alipanda ndege ambayo ilikuwa ikiongozwa na mwanawe Kirubel. Kile alichodhani kuwa ni safari ya kawaida ya kurejea nyumbani kiligeuka kuwa tukio la kihistoria katika maisha yake. Video ya tukio hilo, iliyoanza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kupitia Reddit na baadaye kuripotiwa na vyombo mbalimbali ilionyesha Minalu akipanda ndege huku akiwa hajui chochote kuhusu tukio lilotokea. Baada ya kuketi, mhudumu wa ndege alifungua pazia. Kwa mshangao mkubwa, mama huyo alimwona mwanawe akiwa amesimama ndani ya sare kamili ya rubani, akiwa amebeba shada la maua, keki, na chupa ya mvinyo. Machozi yalimmwagika bila kujizuia. Aliinuka na kumkumbatia Kirubel kwa nguvu, huku abiria wengine wakishuhudia tukio hilo la kipekee kwa hisia kali. #motherslove❤️ #pilot #ethiopianairlines✈️ #aviationcareer #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/reel/DKjTJU_Nyjq/?igsh=MW9zNWJnMG9qN3V1aw== *Mama aliyefanya kazi za ndan...

È una storia che continua a scrivere la sua leggenda: video intervista ad Aldo Ascani per l’apertura dello Shada di Civitanova Marche - MarcheinfiniteÈ una storia che continua a scrivere la sua leggenda: video intervista ad Aldo Ascani per l’apertura dello Shada di Civitanova Marche

di STEFANO FABRIZI - È una storia che continua a scrivere la sua leggenda: video intervista ad Aldo ...