Samia Suluhu Hassan

Samia Suluhu Hassan

737.8K subscribers

Verified Channel
Samia Suluhu Hassan
Samia Suluhu Hassan
January 18, 2025 at 01:38 PM
Mapema leo, nimeungana na wanachama wenzangu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Mkutano Mkuu Maalum hapa mkoani Dodoma. Pamoja na mambo mengine, mkutano huu umemchagua Ndugu Stephen Wasira kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ninampongeza sana, na ni dhahiri kuwa atakuwa na mchango wa kipekee katika kuimarisha utendaji wa chama chetu. Kupitia mkutano huu pia tumepokea na kujadili utekelezaji wa kazi za Chama na Jumuiya zake kwa kipindi cha miaka miwili (2022-2024). Tumesikia juu ya kazi kubwa tunayoendelea kuifanya kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania, na tumeazimia kuwafikia Watanzania wengi zaidi katika maeneo yao, na kutatua changamoto zao katika safari ya kufurahia matunda ya uhuru wetu.
❤️ 🙏 👍 😂 😢 😮 1.0K

Comments