
Samia Suluhu Hassan
January 19, 2025 at 06:13 PM
Shukrani za dhati kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa chama chetu, chama kinachobeba mustakabali wa Taifa letu na imani ya Watanzania, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kuniteua kuwa Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu, 2025.
Sauti yenu na uamuzi wenu ni sauti na uamuzi wa mamilioni ya Watanzania wanaofurahia matunda ya kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Ahadi yangu ni kuendelea na kazi njema ya kuitumikia nchi yetu na Watanzania wote kwa nguvu zote, akili na maarifa yangu yote, wakati wote.
Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa waja wake na Taifa letu aendelee kutusimamia, kutuongoza na kutufanikisha. In'Sha'Allah.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
Mungu Ibariki Tanzania.
❤️
🙏
👍
😢
😂
😮
1.2K