
Samia Suluhu Hassan
January 28, 2025 at 11:19 AM
Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali ya radi iliyosababisha vifo vya wanafunzi 7 na kujeruhi wengine 82 katika Shule ya Sekondari Businda, Wilaya ya Bukombe, Mkoa wa Geita.
Natoa pole kwa Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Naibu wa Waziri Mkuu Mheshimiwa Dkt. Doto Mashaka Biteko, ndugu jamaa na marafiki kwa msiba huu.
Mwenyezi Mungu awarehemu wote waliopoteza maisha katika ajali hii, na awajalie majeruhi wote kupona kwa haraka.
😢
🙏
❤️
👍
😂
😮
1.2K