Samia Suluhu Hassan
January 29, 2025 at 11:47 AM
Pongezi za dhati kwa Baba Askofu Mteule Romanus Elamu Mihali kwa kuteuliwa na Papa Francisko kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Iringa. Uteuzi wako ni ishara ya imani kubwa ya Kanisa kwa utumishi wako. Nakutakia kila la kheri.
Mwenyezi Mungu akushike mkono, akubariki na kukuongoza, unapoendelea kushiriki kazi yake ya kuijenga jamii yetu kuwa bora zaidi katika jukumu hili jipya.
Kutoka: 4:12
“Basi sasa, enenda, nami nitakuwa pamoja na kinywa chako, na kukufundisha utakalolinena.”
🙏
❤️
👍
😢
😮
😂
854