
Samia Suluhu Hassan
February 5, 2025 at 03:49 PM
Kheri ya kumbukizi ya miaka 48 ya kuzaliwa kwa chama chetu, Chama Cha Mapinduzi (CCM). Pongezi kwa Wanachama wetu zaidi ya milioni 12 na mamilioni ya Watanzania wanaovutiwa na sera za CCM, katika siku hii adhimu.
Ahsante kwa waasisi wetu, Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Karume kwa uamuzi wa kihistoria wa kuviunganisha vyama vya TANU na ASP.
Tunasherehekea na kujivunia kazi kubwa iliyofanywa na waasisi wetu, huku CCM ikiendelea kuaminiwa na Watanzania, kushamiri na kutoa uongozi thabiti kwa nchi yetu. Kwa miaka 48, CCM imekuwa chama kinachounganisha watu, kuhubiri umoja, na kutekeleza ahadi zake kwa vitendo katika kuitumikia nchi yetu na watu wake.
CCM inaendelea kuwa tumaini la Taifa letu na Afrika kwa ujumla. Ahadi yetu kwa Watanzania wote ni kuwa CCM imejipanga kuendelea kutoa uongozi thabiti kwa ustawi wa Taifa letu. Pamoja, tuendelee kujenga Taifa letu na kudumisha amani, udugu, upendo na utulivu.
Mungu Ibariki Tanzania.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
❤️
🙏
👍
😂
😢
😮
777