Prime Minister Tanzania

Prime Minister Tanzania

261.2K subscribers

Verified Channel
Prime Minister Tanzania
Prime Minister Tanzania
February 12, 2025 at 04:04 PM
WAZIRI MKUU AKUTANA NA UJUMBE WA WAFANYABIASHARA KUTOKA FALME YA SAUDI ARABIA ▪️Awaeleza mikakati ya Tanzania katika kuvutia wawekezaji. ▪️Awakaribisha kuwekeza kwenye Sekta ya Nishati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji nchini ili kuendelea kuwavutia wawekezaji. Ameyasema hayo leo, (Jumatano 12 Februari 2025) alipokutana na Ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka Falme ya Saidi Arabia, Katika Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu magogoni jijini Dar es Salaam. Mheshimiwa Majaliwa amesema uhusiano baina ya Tanzania na Saudi Arabia umeendelea kuimarika na kufungua fursa kwa wawekezaji kutoka Saudi Arabia kuwa na wigo wa kuwekeza nchini Tanzania hususan katika sekta za nishati, Kilimo, Viwanda, Mifugo Utalii na biashara. Aidha, amesema Tanzania imeendelea kunufaika na fursa ya kusafirisha bidhaa za mazao na mifugo kwenda nchini Saudi Arabia jambo ambalo limeendelea kukuza uchumi wa nchi.
❤️ 👍 🙏 🇹🇿 👏 🔥 😊 32

Comments