Visit Ngorongoro - Tanzania

Visit Ngorongoro - Tanzania

189.1K subscribers

Verified Channel
Visit Ngorongoro - Tanzania
Visit Ngorongoro - Tanzania
January 28, 2025 at 12:11 PM
*NCAA YANADI UTALII NA FURSA ZA UWEKEZAJI MKUTANO WA “AFRICA ENERGY SUMMIT 2025 DAR ES SALAAM.* Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) ni miongoni mwa taasisi za Serikali zinazoshiriki maonesho katika mkutano wa Nishati unaohusisha wakuu wa Nchi za Africa (Africa Energy Summit) ambapo jana umefunguliwa na Naibu Waziri Mkuu, na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko na kuendelea leo tarehe 28, 2025 katika Ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam. Mkutano huo unaowakutanisha wakuu wa nchi zaidi ya 25 barani Afrika, wawakilishi wa wakuu wa nchi na mashirika ya kimataifa ambapo Tanzania ni Nchi mwenyeji umejikita kujadili na kuimarisha sekta ya nishati, jitihada za upatikanaji wa umeme, kuboresha miundombinu ya nishati, na kutafuta suluhu za changamoto zinazokwamisha maendeleo ya sekta hiyo. Vilevile mkutano huo unalenga kuvutia wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi kwenye sekta ya nishati, vyanzo mbadala kama vile jua, upepo, na gesi asilia. NCAA inashiriki mkutano huo kwa ajili ya kutangaza vivuti
👍 ❤️ 4

Comments