WIZARA YA FEDHA - TANZANIA

WIZARA YA FEDHA - TANZANIA

180.2K subscribers

Verified Channel
WIZARA YA FEDHA - TANZANIA
WIZARA YA FEDHA - TANZANIA
February 14, 2025 at 12:40 PM
*ELIMU YA FEDHA YAWAFIKIA WAKAZI WA KATA YA BOMBO- SAME* Baadhi ya wajasiriamali na wananchi kutoka Kijiji cha Mjema, Kata ya Bombo, Tarafa ya Gonja, wakiwa katika Ukumbi wa Ofisi ya Kata ya Bombo pamoja na Timu ya Wataalamu wa Elimu ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Taasisi zake Wilayani Same mkoani Kilimanjaro, wakichangia mada mbalimbali kuhusu elimu ya fedha waliyoipata kupitia njia ya filamu yenye maudhui kuhusu matumizi sahihi ya fedha, umuhimu wa kupanga bajeti na kuitekeleza, umuhimu wa kusajili vikundi vya huduma ndogo za fedha , utunzaji wa fedha binafsi, umuhimu wa kushirikisha familia na watu wa karibu kwenye masuala ya fedha na uwekezaji, umuhimu wa kukata bima ya biashara na mali nyingine. Filamu hiyo imeandaliwa na Wizara ya Fedha ili kusambaza elimu ya fedha kwa njia rahisi ya burudani ili kuhakikisha wananchi wanapata uelewa wa masuala ya huduma za fedha. Hii ni sehemu ya Awamu ya Tatu ya programu inayolenga kuwapa wananchi na wajasiriamali uelewa kuhusu masuala ya fedha. Wilaya za Mwanga na Rombo pia zinatarajiwa kufikiwa na Timu hiyo kama sehemu ya jitihada za kufikisha elimu hii kwa maeneo mengine ya mkoa huo

Comments