Chama Cha Mapinduzi Taifa

Chama Cha Mapinduzi Taifa

82.2K subscribers

Verified Channel
Chama Cha Mapinduzi Taifa
Chama Cha Mapinduzi Taifa
January 26, 2025 at 06:51 PM
WANATAKA MASHINDANO?, WATAENDELEA KUIONA IKULU KWENYE RUNINGA MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stepheni Wasira, amesema vyama vya upinzani kamwe havina uwezo wa kushika dola na vitaendelea kuiona Ikulu kupitia runinga. Wasira aliyasema hayo leo wakati akizungumza na mamia ya wanachama na wapenzi wa CCM walipojitokeza kumpokea jijini Dar es Salaam. "Wanataka mashindano, unawezaje ukashindanisha kijana wa Temeke maskini na Bakhresa?. Hakuna mashindano, unachohitaji ni kumsaidia Bakhresa alafu amsaidie kijana wa Temeke apate maisha bora. "Lakini kuwaambia watashindana, watashindwa kabla ya kuanza mashindano. Ni sawa na kumwambia kiwete ashindane kukimbia na mwenye miguu. Kiwete atashangaa. Kama unataka kuwashindanisha tafuta viwete kwa viwete na wenye miguu kwa wenye miguu. Wasira amesisitiza: "Huwezi kushindanisha vitu visivyofanana. Hiyo ndiyo tofauti yetu na wenzetu na ndiyo maana tunakataa wasishike dola maana watatuharibia. Bahati nzuri Mungu amekataa na dola hawataiona, wataendelea kuiona Ikulu kwenye runinga." #kaziiendelee
❤️ 👍 😂 💚 😮 🙏 🇹🇿 🎓 😏 😭 31

Comments