
TANTRADETANZANIA
February 5, 2025 at 03:39 PM
ETHIOPIA NA TANZANIA KUDUMISHA UHUSIANO WA BIASHARA.
______________
Dar es salaam
04 Februari, 2025
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imepokea ujumbe kutoka ubalozi wa Ethiopia ambao umekuja kwa lengo la kujadili fursa mbalimbali za biashara ikiwa ni pamoja na bidhaa za ngozi na kahawa, zinazopatikana katika nchi ya Tanzania na Ethiopia.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi. Latifa M. Khamis ameahidi ujumbe huo kuwa Mamlaka itatoa ushirikiano ili kujenga mahusiano mazuri ya kibiashara kati ya Tanzania na Ethiopia. Aidha, Mkurugenzi, amewakaribisha kuleta Makampuni ya Ethiopia kushiriki katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam (Sabasaba) yanayotarajiwa kuanza tarehe 28 juni hadi 13 julai 2025 kwa kuwa ni Maonesho yenye manufaa makubwa katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
❤️
👍
🙏
4