Neema Za Dk. Mwinyi
February 12, 2025 at 12:00 PM
RAIS DKT. MWINYI KUKUTANA NA UJUMBE WA WAFANYABIASHARA KUTOKA SAUDI ARABIA
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo tarehe 12 Februari 2025 anatarajiwa kuonana na ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Saudi Arabia, ukiongozwa na Jumuiya ya Wafanyabiashara ya Saudi Arabia, Ikulu Zanzibar.
Wakati huo huo, atashuhudia utiaji saini wa makubaliano ya ushauri kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na Kampuni ya Saudi African Investment and Development Company (SAIDC), pamoja na mkataba wa ushirikiano kati ya Jumuiya ya Kitaifa ya Wafanyabiashara Zanzibar (ZNCC) na Shirikisho la Vyama vya Wafanyabiashara la Saudi Arabia, kwa lengo la kuimarisha uwekezaji wa kimkakati na kukuza uchumi wa Zanzibar.
Ujio wa ujumbe huo umetokana na Kongamano la Biashara na Uwekezaji lililofanyika mwezi Desemba 2024 jijini Riyadh, Saudi Arabia, ambalo liliwashirikisha watendaji wakuu wa Serikali ya SMZ na SMT.
📅 12 Februari 2025
📍Ikulu Zanzibar
❤️
1