
Idara ya Habari - MAELEZO na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali
January 24, 2025 at 02:44 PM
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Ndg. Gerson Msigwa leo Januari 24, 2024 amesafiri kwa usafiri wa Treni ya Reli ya Kisasa (SGR) pamoja na Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Dodoma kutoka mkoani humo kuelekea Morogoro ambapo wataungana na Waandishi wa Habari wa Morogoro kwa ajili ya Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Serikali utakaofanyika Jumamosi, Januari 25, 2025 katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.