Idara ya Habari - MAELEZO na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali
Idara ya Habari - MAELEZO na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali
January 29, 2025 at 10:56 AM
SHUKRANI. Kwa dhati naomba kuwashukuru Waandishi wa Habari wenzangu wa Vyombo vya Habari vya Kitaifa na Vyombo vya Habari vya Kimataifa kwa namna mlivyoitikia kuutangaza Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi Barani Afrika uliofanyika tarehe 27-28 Januari, 2025. Mmefanya kazi kubwa kabla, wakati na baada ya mkutano ambapo mmeandika makala, habari za matukio, vipindi vya redio na televisheni zaidi ya 1,040 vilivyochapishwa katika vyombo vya habari ndani ya Nchi na vya Kimataifa. Mfumo wetu wa ufuatiliaji na tathmini umeonesha taarifa za mkutano huu zimesomwa, zimesikikizwa na kutazamwa na Mamilioni ya watu Duniani kote na zinaendelea kusomwa, kusikilizwa na kutazamwa. Tulibarikiwa kuwa na Waandishi wa Habari wa vyombo vya habari vya Kimataifa zaidi 70 na wa vyombo vya habari vya ndani ya nchi zaidi ya 150. Kazi yenu kubwa itachochea wadau wengi zaidi kujitokeza na kuungana na Afrika katika safari ya kuwaunganishia umeme Waafrika zaidi ya Milioni 300 ifikapo mwaka 2030. Viongozi wetu wanaendelea kupokea wadau waliotayari kumaliza changamoto ya nishati ya umeme na kuwawezesha Waafrika kutumia nishati safi ya kupikia kama ambavyo mkutano ulilenga. Nawaombeni tuendelee kushirikiana katika matukio mengine mengi yanayokuja, hasa wakati huu ambapo Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kufanya mambo makubwa ya kuipeleka Tanzania katika uchumi mkubwa zaidi wenye kugusa maisha ya watu moja kwa moja. Pia, nawashukuru watu wote ambao mlitenga muda wenu kufuatilia mkutano huu ili kujua jitihada zinazofanywa na Serikali kukabiliana na changamoto za Waafrika na watu wote wanaokujua Afrika kuwekeza na kuishi. Mwenyezi Mungu awabariki sana. Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo & Msemaji Mkuu wa Serikali. #kaziiendelee
❤️ 👍 🙏 3

Comments