
Idara ya Habari - MAELEZO na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali
February 3, 2025 at 03:11 PM
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kupokea tuzo ya “The Gates Goalkeepers Award” kama kielelezo cha matokeo makubwa ambayo yamepatikana kwenye uongozi wake kufuatia ripoti ya utafiti wa demografia na afya ya mwaka 2022 inayoonesha kupungua kwa vifo vitokanavyo na uzazi kwa asilimia 80.
Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama amesema hayo Februari 3, 2025 wakati akitoa taarifa ya upokeaji wa tuzo hiyo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan zinazoandaliwa na taasisi ya The Gates Foundation, mbele ya waandishi wa habari kwenye ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
👏
1