WIZARA YA FEDHA - TANZANIA

WIZARA YA FEDHA - TANZANIA

180.2K subscribers

Verified Channel
WIZARA YA FEDHA - TANZANIA
WIZARA YA FEDHA - TANZANIA
February 17, 2025 at 07:17 AM
*KATA YA KILEO-MWANGA NA ELIMU YA FEDHA* Baadhi ya wajasiriamali na wananchi kutoka Kata ya Kileo, Wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro, wakiwa katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Kifaru wakiwa pamoja na Timu ya Wataalamu wa Elimu ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Taasisi zake, wakichangia mada mbalimbali kuhusu elimu ya fedha waliyoipata kupitia njia ya filamu yenye maudhui kuhusu matumizi sahihi ya fedha, umuhimu wa kupanga bajeti na kuitekeleza, umuhimu wa kusajili vikundi vya huduma ndogo za fedha , utunzaji wa fedha binafsi, umuhimu wa kushirikisha familia na watu wa karibu kwenye masuala ya fedha na uwekezaji, umuhimu wa kukata bima ya biashara na mali nyingine. Filamu hiyo imeandaliwa na Wizara ya Fedha ili kusambaza elimu ya fedha kwa njia rahisi ya burudani ili kupunguza utegemezi na kudhibiti fedha zao katika jamii. Aidha, Elimu ya fedha itawasaidia wananchi kutengeneza mipango ya kifedha ya muda mrefu, ambayo imejumuisha kujiandaa kwa dharura, kujenga akiba, na kupunguza hatari za kifedha zinazoweza kutokea kama magonjwa au ajali

Comments