
Samia Suluhu Hassan
February 23, 2025 at 05:03 PM
Baada ya kazi Dar es Salaam, alasiri niliwasili mkoani Tanga kuanza ziara yangu ya kikazi, ambapo pamoja na mambo mengine nitazindua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi.
Kati ya mwaka 2021 hadi mwanzoni mwa mwaka huu, Serikali imeupa Mkoa wa Tanga takribani Shilingi Trilioni 3.1 kwa ajili ya utekelezaji miradi ya maendeleo, ambapo Shilingi Bilioni 65.6 kati ya hizo zimekwenda kwenye Sekta ya Afya.
Wananchi wamepata ahueni kubwa ya maisha kutokana na matokeo ya miradi hii, ikiwemo Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni inayohudumia vijiji 91. Mbali na huduma nyingine za kitabibu, tumefanikiwa kuiwezesha hospitali hii kuwa na vifaa muhimu vya kutunzia watoto njiti, na leo nimefarijika kuona baadhi yao wakiendelea na matibabu.
❤️
🙏
👍
😂
😢
😮
570