Samia Suluhu Hassan
                                
                                    
                                        
                                    
                                
                            
                            
                    
                                
                                
                                February 24, 2025 at 06:48 PM
                               
                            
                        
                            Imekuwa Jumatatu nzuri ya kazi na wananchi Bumbuli, Lushoto Mjini, Mkomazi na kisha Korogwe Mjini, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yangu ya kikazi katika Mkoa wa Tanga. 
Mbali na kuupa Mkoa wa Tanga Shilingi Trilioni 3.1 kwa miradi ya maendeleo katika kipindi cha miaka minne ambayo sasa tunaona matokeo yake kwenye maisha ya wananchi, tumeanza ujenzi wa Bwawa la Umwagiliaji Mkomazi, moja ya miradi muhimu kwa watu wa Mkoa wa Tanga hasa kwenye kilimo. Katika Wilaya ya  Korogwe pekee, mradi huu utanufaishi zaidi ya wananchi 20,000, na kuwapa nafasi ya kukua zaidi katika kilimo cha mazao ya chakula na biashara.
                        
                    
                    
                    
                    
                    
                                    
                                        
                                            ❤️
                                        
                                    
                                        
                                            🙏
                                        
                                    
                                        
                                            👍
                                        
                                    
                                        
                                            😂
                                        
                                    
                                        
                                            😢
                                        
                                    
                                        
                                            😮
                                        
                                    
                                    
                                        606