Samia Suluhu Hassan

Samia Suluhu Hassan

737.8K subscribers

Verified Channel
Samia Suluhu Hassan
Samia Suluhu Hassan
February 25, 2025 at 07:50 PM
Nimekuwa na wakati mzuri na wananchi katika Wilaya ya Kilindi na kisha Mji wa Handeni, ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yangu ya kikazi katika Mkoa wa Tanga. Pamoja na miradi mingine mikubwa ambayo tunaendelea kutekeleza katika maeneo haya, leo nimeweka Jiwe la Msingi katika Mradi wa Maji wa Miji 28 kama sehemu ya kazi kubwa tunayofanya ya kumaliza changamoto ya maji safi na salama kwa wananchi takribani milioni moja ndani ya Wilaya za Handeni, Korogwe, Muheza na Pangani.
❤️ 🙏 👍 😂 😢 😮 474

Comments