Samia Suluhu Hassan
February 26, 2025 at 12:08 PM
Wilaya kwa wilaya katika kazi, nikiendelea na ziara yangu katika Mkoa wa Tanga ambapo pamoja na mambo mengine, nchi yetu imeandika historia ya kujivunia katika miundombinu nilipoweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Daraja la Mto Pangani (Urefu wa mita 525) na Barabara ya Bagamoyo (Makurunge) - Saadani, na Tanga – Pangani (Kilomita 256).
Baada ya jambo hili la kihistoria kwa nchi yetu, na kabla ya kuanza safari yangu ya kutoka Pangani kuelekea katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Tanga Mjini, nimezindua rasmi ugawaji wa boti kubwa za kisasa 120 pamoja na boti saidizi 118 kwa nchi nzima. Katika ugawaji wa boti hizi, nimekabidhi boti kubwa 30 na boti saidizi 60 kwa Mkoa wa Tanga.
❤️
🙏
👍
😂
😢
😮
474