
Radio Maria Tanzania
March 1, 2025 at 03:57 AM
LEO MACHI 1 TUNAYAKUMBUKA MAISHA YA MTAKATIFU SWITBERTI, ASKOFU (713)
Maisha ya Switberti ni kielelezo bora kukusia matatizo katika maisha ya wamisionari, matatizo ya usafiri katika nchi za misioni na vikwazo vilivyokuwepo kutokana na vita vya makabila ambayo wakati mwingine huharibu ushindi wa mwanzo wa kueneza Injili.
Switberti ni mmojawapo wa kikundi cha wamisionari kumi na wawili Waingereza na Waairishi walioongozwa na Mtakatifu Wilibrodi ( tunayemkumbuka Novemba 7) Wamisionari hao, walitoka Uingereza Mwaka 690, wakavuka Bahari ya Kaskazini, wakaanza kueneza Injili kwa Wafrisi, kabila linaloishi Uholanzi na Ujerumani.
Baadaye, walielekea upande wa kusini
wakitembea umbali mrefu kwenye nchi kavu kwa kufuata mto wa Rain.
Hii ilikuwa shughuli kubwa sana kwa wakati ule. Walipata shida nyingi na walivikabili vizuizi vingi, lakini mwishoni walifanikiwa, wakaanza kuhubiri na kufundisha katika sehemu zile.
Mtakatifu Switberti aliwaingiza watu wengi katika dini kwa utamu wa maneno yake.
Kwa sababu Wamisionari
wenzake walimchagua kuwa Askofu, Mtakatifu Switberti aliamua kurudi Uingereza kutafuta wamisionari wengi zaidi na akiwa nyumbani alipewa daraja ya Uaskofu.
Kabla ya kurudi Uingereza, alimwachia Mtakatifu
Wilibrodi kazi ya kuyaangalia Makanisa aliyokuwa amekwisha kuyafungua.
Askofu Switberti aliporudi Ujerumani tena, baada ya kupewa Uaskofu, alipenya zaidi katika nchi na aliwabatiza watu wengi wa makabila mengine. Lakini kwa bahati mbaya sana, miaka michache baadaye kabila la Wasaksoni waliiteka na kuishikilia nchi na hivyo kazi yake iliharibiwa sana.
Askofu Switberti alikimbilia katika kisiwa kimoja huko mto Rain na kujitayarisha kwa kifo chake.
Alijenga nyumba ya Kitawa huko na alikufa hapo hapo kwenye nyumba hiyo.
Mwaka 713, Masalia yake yaliwekwa kwenye sanduku ambalo baadaye lilipotea. Lakini baada ya miaka 900 likapatikana tena.
MTAKATIFU SWITBERTI, ASKOFU UTUOMBEE.
#radiomariatanzania
#injlishakwaharaka
#mahujajikatikamatumaini

🙏
❤️
👍
🥰
29