Hussein Ali Mwinyi

Hussein Ali Mwinyi

102.8K subscribers

Verified Channel
Hussein Ali Mwinyi
Hussein Ali Mwinyi
February 26, 2025 at 02:44 PM
RAIS MWINYI:TUWASAIDIE MAIMAMU NA WALIMU WA MADRASA Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewasisitiza Waumini wa Dini ya Kiislamu kuwa tayari kuwasaidia Maimamu na Walimu wa Madrasa kwa hali na Mali ili wawe na hali Bora za kimaisha na kuendelea kufundisha Elimu ya Dini kwa Ufanisi. Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipoufungua Msikiti wa Almaghafira uliopo Nungwi Kidimni, Mkoa wa Kaskazini Unguja. Akizungumza na Waumini wa Dini ya Kiislamu amewahimiza Kuutumia Msikiti huo kwa Kusali kwa Bidii pamoja na kuandaa Utaratibu Mzuri wa Kuutunza ili ubaki kuwa na Mazingira mazuri wakati wote. Msikiti wa Almaghafira uliojengwa kwa Nguvu za Waumini na Wahisani mbali mbali.
❤️ 🙏 👍 9

Comments