
Prime Minister Tanzania
February 22, 2025 at 07:45 PM
*WAZIRI MKUU ASHIRIKI MAZIKO YA BI. ASINA OMARI*
WAZIRI MKUU na Mbunge wa Jimbo ya Ruangwa Mheshimiwa Kassim Majaliwa leo Februari 22, 2025 ameshiriki katika mazishi ya marehemu Bi. Asina Omary Nyimbilile mkazi wa Kata ya Nkowe, Ruangwa mkoani Lindi.
Akizungumza na waombolezaji katika mazishi hayo, Mheshimiwa Majaliwa amewataka ndugu, jamaa na marafiki kumuombea Marehemu Bi. Asina pumziko la milele pamoja na kuyaenzi yote mema aliyofanya wakati wa uhai wake.
Bi. Asina amezikwa katika makaburi ya jumuiya yaliyopo katika kata ya Nkowe.
Mazishi hayo pia yamehudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Ndugu Hassan Jarufu, Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Hassan Ngoma na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ruangwa Ndugu Ibrahim Ndoro.
😢
❤️
👍
😭
🙏
🫡
7