
Tech & Media Convergency (TMC)
February 26, 2025 at 05:50 PM
📍VIDEO:
Shirika la Tech and Media Convergency (TMC) @MediaConvergecy, kwa kushirikiana na wadau wa habari na mashirika ya kimataifa kama @UNESCO, limezindua ripoti muhimu kuhusu matumizi ya Akili Mnemba (Artificial Intelligence - AI) katika sekta ya habari.
Ripoti hiyo imekusanya maoni ya waandishi wa habari na wadau mbalimbali ili kubaini mapokeo, changamoto, na fursa zinazotokana na teknolojia hiyo mpya.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa TMC, Asha Abinallah, amesema kuwa ripoti hiyo imezingatia maeneo manne muhimu: ubunifu, teknolojia, matokeo na ushirikiano.
Amesisitiza kuwa maendeleo ya kidijitali yameleta mabadiliko makubwa katika uandishi wa habari, na hivyo ni muhimu kwa waandishi na wahariri kujiandaa ipasavyo kuendana na mabadiliko hayo.
"Ubunifu siku hizi unategemea kwa kiasi kikubwa teknolojia. Waandishi wa habari wanapaswa kuelewa na kukubali (AI) kama sehemu ya maisha yao ya kila siku na nyenzo ya kuboresha utendaji wao," alisema Bi. Asha
👍
🕹️
2