Tech & Media Convergency (TMC)
Tech & Media Convergency (TMC)
February 26, 2025 at 05:51 PM
Katika juhudi za kuimarisha matumizi ya AI, TMC imefanya ushirikiano na mashirika kama Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC). Kupitia mradi huo, waandishi 300 wanatarajiwa kupata mafunzo maalum kuhusu matumizi ya AI katika kazi zao. Aidha, Bi. Asha, ameeleza kuwa ukusanyaji wa maoni kutoka kwa wadau umewezesha kubaini changamoto zinazowakabili waandishi katika kutumia teknolojia mpya. Hii imesaidia kuandaa mwongozo wa mafunzo ili kuhakikisha kuwa maeneo yenye changamoto yanashughulikiwa kwa kina. "Tunataka kuhakikisha waandishi wa habari wanakuwa na uelewa sahihi wa AI na namna inavyoweza kuboresha uandishi wa habari, huku tukihakikisha matumizi yake yanakuwa na matokeo chanya kwa jamii," aliongeza. Kwa kuzingatia kuwa Tanzania ina waandishi wa habari takriban 3,000, ripoti hii ni hatua muhimu kuelekea mapinduzi ya kidijitali katika sekta ya habari, huku AI ikichukuliwa kama nyenzo muhimu ya kuimarisha ufanisi wa uandishi na uhariri wa habari. Cc: Jambo Tv
❤️ 👍 🕹️ 4

Comments