
Tech & Media Convergency (TMC)
February 27, 2025 at 11:08 AM
DAR-ES-SALAAM : MWENYEKITI wa Bodi ya Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Joyce Shebe, amevishauri vyombo vya habari kutumia teknolojia ya akili mnemba (AI) kwa uhakiki wa taarifa kabla ya kuzichapisha kwa umma.
Akichangia matokeo ya utafiti kuhusu matumizi ya teknolojia ya AI kwa maendeleo ya vyombo vya habari uliofanywa na Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na maendeleo ya Tehama nchini, TMC, Joyce amesema kuwa inasikitisha kuona baadhi ya vyombo vya habari vikiendelea kuchapisha taarifa za upotoshaji, jambo linaloweza kuathiri maendeleo ya nchi.
“Maendeleo ya teknolojia ya AI yamepunguza mzigo wa kazi na kurahisisha utekelezaji wa majukumu. Vyombo vya habari vinapaswa kutumia fursa hii kwa umakini ili kuepuka uenezaji wa taarifa za uongo,” alisema Joyce.
Imeandaliwa : Kulthum Ally
👍
1