
MwinyiApp
February 23, 2025 at 07:48 AM
Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewaahidi wananchi kuwa bidhaa muhimu zitakuwepo kwa wingi wakati wa mwezi wa Ramadhani, na Serikali itahakikisha usambazaji mzuri wa bidhaa na usimamizi wa bei ili kuepusha mfumuko wa bei. Alisisitiza umuhimu wa wafanyabiashara kutoa huduma bora kwa bei nafuu, huku akiwataka Wazanzibari kudumisha mshikamano, kusaidiana, na kuonyesha huruma kwa wale wanaohitaji msaada. Dkt. Mwinyi pia amewatakia Waislamu mwezi mtukufu wa Ramadhani wenye amani na mafanikio.
#mwinyiapp
#yajayonineemazaidi
#dumishaamaniazanzibar
