MwinyiApp
MwinyiApp
February 23, 2025 at 08:29 AM
Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amezindua rasmi Zanzibar SUKUK na kusema kuwa utaratibu huu wa hati fungani ni hatua muhimu ya kufikia maendeleo endelevu kwa kuzingatia misingi ya Sharia. Dkt. Mwinyi alifafanua kuwa SUKUK itasaidia Serikali kupata fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mingi inayokusudiwa katika muda mfupi ujao, huku ikitoa fursa kwa wananchi, wadau, na taasisi mbalimbali kupata faida ya asilimia 10.5 kila mwaka. Aidha, Rais Mwinyi alisisitiza kuwa mafanikio ya SUKUK yanahitaji ushiriki wa wananchi wengi na kukanusha taarifa potofu kuhusu kuuza Benki ya Watu wa Zanzibar, akieleza kuwa lengo ni kuijengea uwezo ili iwe na mtaji mkubwa wa kufadhili miradi ya maendeleo. #mwinyiapp #yajayonineemazaidi #dumishaamaniazanzibar
Image from MwinyiApp: Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amezindua rasmi Zanzibar SU...

Comments