
MwinyiApp
March 1, 2025 at 12:04 PM
Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amebainisha kuwa Zanzibar itaongeza idadi ya watalii kutoka Asia kwa kuboresha miundombinu ya utalii, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa hoteli za kisasa, uimarishaji wa viwanja vya ndege, na huduma bora za usafiri. Dkt. Mwinyi alisema kuwa mikakati hii inalenga kuvutia wageni kutoka Asia, hasa kutokana na mazingira ya kuvutia ya Zanzibar, utamaduni wake wa kipekee, na fukwe nzuri. Alisisitiza kuwa sekta ya utalii ni muhimu katika kukuza uchumi wa Zanzibar, na juhudi hizi zitasaidia kufanikisha malengo ya kuongeza mapato na ajira kwa wananchi.
#mwinyiapp #yajayonineemazaidi #dumishaamanizanzibar
