
MwinyiApp
March 1, 2025 at 12:14 PM
Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesisitiza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na Kampuni ya Vodacom Tanzania katika kuharakisha huduma za kidigitali nchini. Akizungumza alipokutana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania, Philip Besiimire, Dkt. Mwinyi alisisitiza umuhimu wa ushirikiano huu katika kuboresha sekta muhimu za elimu, afya, na maendeleo ya kijamii. Kwa upande mwingine, Besiimire alieleza kuwa Vodacom itapanua huduma zake Zanzibar kupitia miundombinu ya kidijitali na kusaidia vijana na wanawake kwa ujuzi wa kidijitali na kifedha. Vodacom pia imeahidi kuunganisha zaidi ya shule 100 Zanzibar ifikapo 2026 kupitia Foundation yake, ili kuboresha ufundishaji wa kielektroniki.
#mwinyiapp #yajayonineemazaidi #dumishaamanizanzibar

🙏
1