
World Affairs Today 🌎
February 9, 2025 at 09:56 PM
*Nadharia ya Kinajma (Conspiracy Theory) ni maelezo yanayodai kuwa matukio fulani yanatokana na mipango ya siri inayotekelezwa na vikundi vya watu wenye nguvu kwa malengo ya kificho. Nadharia hizi mara nyingi hukosa ushahidi wa moja kwa moja na zinatilia shaka simulizi rasmi kuhusu matukio fulani.*
_*Ulinganisho na Tukio la 9/11_*
Mashambulizi ya Septemba 11, 2001 (9/11) nchini Marekani yalihusisha ndege nne za abiria zilizodaiwa kutekwa nyara na magaidi wa al-Qaeda, ambapo mbili ziligonga majengo ya World Trade Center (WTC) jijini New York, moja ikalenga Pentagon, na ya nne ikaanguka Pennsylvania baada ya abiria kujaribu kuudhibiti.
*Baadhi ya nadharia za kinajma kuhusu 9/11 zinadai kuwa:*
1. Serikali ya Marekani ilihusika – Baadhi ya watu wanaamini kuwa mashambulizi haya yaliruhusiwa au hata kupangwa na serikali ili kutoa sababu ya kushambulia nchi za (Justfy War) Kiislamu kama Iraq na Afghanistan.
2. Majengo ya WTC yalilipuliwa kwa makusudi – Wengine wanadai kuwa mnara wa Kati wa Biashara Ulimwenguni (Twin Towers) haukuanguka kutokana na mgongano wa ndege pekee bali ulilipuliwa kwa milipuko ya ndani.
3. Ndege iliyogonga Pentagon haikuwa ndege ya abiria – Kuna wanaoamini kuwa hakuna ushahidi wa kutosha wa kuonyesha kuwa ndege ya abiria iligonga jengo hilo, bali kombora lilirushwa kwa makusudi.
4. Mfumo wa ulinzi wa Marekani ulikuwa na taarifa lakini haukuchukua hatua – Kuna madai kuwa maafisa wa serikali walikuwa na onyo la mapema kuhusu shambulizi lakini waliliacha litokee kwa malengo fulani ya kisiasa.
USHAHIDI KAMILI UPO
cont.........