
Salva Media Tanzania
February 10, 2025 at 11:23 PM
Kendrick Lamar ndio jina linalovuma zaidi kwenye mitandao ya kijamii hii inakuja baada ya msanii huyo kushiriki katika matukio makubwa ndani ya wiki moja pekee.
Tukio la kwanza - Ni kuibuka kama mshindi bora katika tuzo za GRAMMY 2025
Tukio la pili ni kutumbuiza katika kilele cha NFL Superbowl 2025.
Ukiingia mtandao wa X jina la Kendrick Lamar limechukua nafasi ya kwanza katika majina yaliyotafutwa sana ndani ya saa 24.
Kwenye mitandao mingine kama Instagram, video na picha zake zimewekwa na kurasa nyingi.
https://youtube.com/shorts/zVZbjsupwNk?feature=share