Pamoja Mapendano Serge PMS
Pamoja Mapendano Serge PMS
February 19, 2025 at 08:03 PM
BONSOIR WANDUGU KATIKA KRISTO. TUSOME VIZURI MAANDIKO MATAKATIFU HIZI NA TUZITIYE KWA TENDO NDANI YA MA GROUPES ZETU MITANDAONI NA POPOTE TAFAZILI, TUFANYE HIVYO KWA JINA LA YESU. Biblia Takatifu 👇🏾👇🏾👇🏾 Wakolosai 3:8-10,12-17 [8]Lakini sasa yawekeni mbali nanyi haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano, na matusi vinywani mwenu. [9]Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake; [10]mkivaa utu mpya, unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba. [12]Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, [13]mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi. [14]Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu. [15]Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani. [16]Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. [17]Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye. ✍🏿PMS

Comments