
SAHIHI TV
February 6, 2025 at 02:29 PM
Waasi wa M23 wameunda Serikali mpya nchini DRC kwa kumteua Kanali Bahati Musanga kuwa Gavana wa Jimbo la Kivu Kaskazini, manaibu Gavana wawili, Willy Manzi na Shadary Bahati, Meya wa Jiji la Goma, pamoja na Wakuu wa Wilaya.
M23 imetangaza uteuzi huo wiki moja baada ya kuuteka mji wa Goma, huku sehemu kubwa ya maeneo mengine yakiwemo eneo kubwa la Walikale, Lubero, na Beni yakiwa bado chini ya udhibiti wa serikali ya DRC.