SAHIHI TV
SAHIHI TV
February 7, 2025 at 04:54 AM
Jaji wa Marekani amesitisha kwa muda mpango wa Rais Donald Trump wa kutoa motisha kwa wafanyikazi wa shirikisho kujiuzulu kwa hiari kabla ya makataa ya Alhamisi usiku wa manane. Jaji wa shirikisho George O'Toole Jr alisema mpango huo utasitishwa hadi kesi itakaposikilizwa siku ya Jumatatu ambapo ataweza kubaini uhalali wa kesi iliyowasilishwa na vyama vya wafanyakazi vya serikali, limeripoti shirika la habari la CBS, mshirika wa BBC wa Marekani. Mpango wa kuwalipa wafanyakazi wanaojiuzulu kwa hiari ni sehemu ya juhudi zinazoendelea za utawala wa Trump za kupunguza ukubwa wa serikali ya shirikisho. Ikulu ya Marekani inasema zaidi ya wafanyakazi 40,000 wamekubali ombi la kujiuzulu ili wapate malipo hadi kufikia tarehe 30 Septemba. Baadhi ya wafanyikazi wametoa maoni ya mkanganyiko kuhusu masharti ya mpango huo. #keyter

Comments