
SAHIHI TV
February 7, 2025 at 11:24 AM
Mahakama ya Kijeshi nchini DRC imetoa hati ya kukamatwa kwa kiongozi wa umoja wa makundi ya waasi nchini humo ya Alliance Fleuve Congo (AFC/M23), Corneille Nangaa kwa tuhuma za uasi na uhalifu wa kivita dhidi ya raia nchini humo.
Vyombo vya Habari vya serikali DRC vimeripoti kuwa hati ya kukamatwa kwa Nangaa imetolewa baada ya kuhusika katika mauaji ya maelfu ya raia katika mapigano yaliyoibuliwa na wapiganaji wake Kivu Kaskazini nchini humo.
Mahakama hiyo imeamuru Nangaa akamatwe akiwa mahali popote atakapokutwa duniani na kufikishwa katika Mahakama ya Kijeshi nchini DRC.#keyter