
SAHIHI TV
February 12, 2025 at 06:19 AM
Rais Donald Trump kwa mara nyingine amesisitiza kuwa Marekani itachukua udhibiti wa Ukanda wa Gaza, alipokutana na Mfalme Abdullah wa Jordan katika Ikulu ya White House siku ya Jumanne.
Ulikuwa ni mkutano wao wa kwanza tangu Trump atangaze pendekezo lake la kuchukua eneo hilo na kuwahamisha Wapalestina milioni mbili katika nchi nyingine za eneo hilo, ikiwemo Jordan.
Mapema wiki hii, Trump alipendekeza kuwa anaweza kuzuia msaada kwa Jordan na Misri isipokuwa wakubali kuwachukua Wapalestina hao kutoka Gaza.
Jordan, mshirika mkuu wa Marekani katika Mashariki ya Kati, tayari ni nyumbani kwa mamilioni ya Wapalestina na imekataa pendekezo hilo. Mfalme Abdullah alisema baada ya mkutano wao kwamba "msimamo thabiti wa Jordan [ni] dhidi ya kuhama kwa Wapalestina".
Lakini akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi ya Oval, huku Mfalme Abdullah akiwa ameketi upade wake wa kulia, Trump aliashiria hatabadili wazo lake ambalo lilizua shutuma za kimataifa alipolizindua wiki iliyopita.
"Tutaichukua. Tutaishikilia. Tutaienzi," alisema kuhusu Gaza.#keyter