
Injili All Over The World
February 17, 2025 at 11:06 AM
NENO LA MUNGU NI UPANGA
SI KILA UNAPOLISIKIA UJISIKIE RAHA KAMA UNAPAKWA PODA, UTACHELEWA, KUNA MUDA NI MAUMIVU UKILISIKIA LAKINI UKILIRUHUSU HALIKUACHI NA MAUMIVU, YANI LINAKUKATAKATA HALAFU LINAKUSHUGHULIKIA KUFUNGA KIDONDA NA KUKUPONYA HAPOHAPO
Hebrews 4:12
[12]For the word of God is quick, and powerful, and sharper than any twoedged sword, piercing even to the dividing asunder of soul and spirit, and of the joints and marrow, and is a discerner of the thoughts and intents of the heart.
Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
TUANGALIE MFANO WA KUTENGENEZA FURNITURE/SAMANI
TUNAANZA KUKATA MITI(WAKATI HUO UNAHESABIKA KAMA UHARIBIFU)
BAADA YA HAPO MTI UNAONDOLEWA MAGANDA YA NJE
MBAO INACHANWACHANWA
WANAITENGENEZA TENA ILI IWE SOFT KISHA WANATENGENEZA FURNITURE AMBAYO INAGONGWAGONGWA NA MISUMARI NA NYUNDO,
UNAWEZA KUONA HIZI BUGHUDHA HUU MTI UNAPITIA HADI KUFANYA SAMANI NZURI UKIITAZAMA UNASEMA WOOOOOW, LAKINI UKIKUTA NDIO KWANZA MTI UNAKATWA AU INACHANWA MBAO UNAWEZA KUONA SI KITU CHA KUVUTIA.
MCHAKATO UNAWEZA USIKUVUTIE SANA, SAMANI ITAKUVUTIA, SAMANI ZINA BEI KUBWA TENA KULINGANA NA AINA YA MTI NA UJUZI WA FUNDI KUTOA KILICHO BORA
MTI TUKIUPENDA TUSIPOUKATA HATUPATI SAMANI
MTI USIPOCHANWA MBAO HATUPATI SAMANI
MTI USIPOGOMGWA NA NYUNDO NA MISUMARI HATUPATI SAMANI
ACHANA NA HIZI SAMANI ZA KICHINA WANACHUKUA UNGA WA MBAO WANATENGENEZA SAMANI WANAUNGANISHA NA GUNDI, WIKI MBILI NYINGI KILA KIPANDE KINAANZA KUJITEGEMEA.
MCHAKATO HUU NDIO MCHAKATO WA NENO KWA MTU, PANGA/SHOKA BUTU HALIWEZI KUKATA MTI MGUMU, TUNAHITAJI PANGA/ MSUMENO MKALI
LEO TUNAPUNGUZA MAKALI YA NENO, JE HATUTAKI KIBURI(MITI) NDANI YETU IKATWE IANGUKE KISHA TUANZE KUSHUGHULIKIWA STYLE YA KUCHANA MBAO, TUBAMIZWE DESIGN YA NYUMDO NA MISUMARI, TUTIWE POLISH TUNG'ARE?
⚠️MADHARA YA NENO KUPUNGUZWA UKALI NI YAPI
.UBORA WA MATOKEO YA INJILI AU NENO UNABAKI STORY NA SI UHALISIA
.KINAINUKA KIZAZI CHA WAPAGANI WANAOLITAJA JINA LA MUNGU/YESU
.MAPENZI YA MUNGU HAYATIMII. KAZI YA NENO NI KUTIMIZA MAPENZI YA MUNGU. LINAVYOKWENDA KINYUME NA LILIVYOACHILIWA BASI HAKINA MAPENZI YA MUNGU
.MAUTI, KWENYE NENO KUNA UZIMA, KUPUNGUZA MAKALI YA NENO NI KUPUNGUZA KIWANGO CHA KUISHI. NI KUANZA KUFA TARATIBU NA MWISHOWE KUFA KABISA
💥 KWELI NDIYO INAWEKA WATU HURU TENA KWELI YOTE NA SI KWELI KIDOGO
💥KWELI UNAYOFAHAMI ITAKUFIKISHA UKOMO AMBAPO KWELI ULIYOFICHWA INGEKUSAIDIA KWENDA MBELE
📌USIWE MUAMBIWA UKWELI TU, KAZANA KUITAFUTA KWELI NI IPI KUHUSU MUNGU NA NENO LAKE JUU YA MAISHA YAKO
❌ANAPOELEZWA MTU UKWELI USITETEE KWA SABABU INATOA KIBURI KWA MUHUSIKA. NEXT TIME ATAFANYA ZAIDI HATA UNAYETETEA UTAKUWA DISAPPOINTED.
INJILI HATA KAMA INAUMA KIASI GANI, IPOKEE NDIO UNABAMIZWA HAPO BIDHAA IPATIKANE, HUTAKUWA WEWE KAMA HUTAKUBALI NENO LIKUTENGENEZE,,