AGA KHAN HEALTH SERVICE, TANZANIA
AGA KHAN HEALTH SERVICE, TANZANIA
February 8, 2025 at 04:43 PM
Tumefarijika na ujio wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Albert Chalamila, hapa Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam, kutoa salamu za rambirambi katika msiba wa Mtukufu Aga Khan IV, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Mkuu wa Mkoa aliongozana na Dkt. Mohammed Mang’una, Mganga Mkuu wa Mkoa, na Dkt. Toba Nguvila, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, na kupokelewa na uongozi wa Taasisi ya Huduma za Afya ya Aga Khan, Tanzania. Tunatoa shukrani za dhati kwa ujio huu na ushirikiano tulioupata katika kipindi hiki kigumu. Mkuu wa Mkoa pia alimsifu hayati kwa uongozi wake bora na juhudi za kuleta maendeleo, akimwona kama kiongozi bora, shujaa wa kuleta maendeleo, na mshirika mwaminifu ambaye aliwekeza katika kusaidia jamii ya Tanzania kupitia sekta mbalimbali, ikiwemo huduma za Afya, Shule, na vyuo vikuu. Mchango wake utaendelea kunufaisha watanzania.
❤️ 1

Comments